Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Mgomo waja Reli ya kati.

Chama cha Wafanyakazi wa Reli ya Kati (TRAWU) kimechimba mkwara kwa uongozi wa Shirika la Reli (TRL) kuongeza mishahara katika muda huo vinginevyo watagoma.

Katibu wa TRAWU, Bw. Sylivester Rwegasira, aliwaambia wandishi wa habari wametoa muda wa saa 48 ili uongozi wa TRL utoe uamuzi.

Bw. Rwegasira alisema miaka 10 kabla ya kuingia mbinu mpya, Shirika la Reli Tanzania (TRC) lilikuwa likiwapiga danadana wafanyakazi wake inapofikia hatua ya kuongeza mishahara, huku wakidai kuwa nyongeza hiyo itafanyika baada ya kuingia mwekezaji huyo.

Alisema tangu Januari mwaka huu, wafanyakazi walitaka kugoma, lakini TRAWU iliwashawishi waendelee na kazi wakati majadiliano yakiendelea lakini hakuna kilichofanyika.

Alisema madai hayo yalifikishwa Wizara ya Kazi, Maendeleo ya Vijana na Ajira, lakini hakuna ufumbuzi wa kuongezwa mishahara uliofikiwa.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.