Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Aga Khan Kriketi iko juu

Hatimaye Timu ya Kriketi ya Aga Khan imeweza kutwaa ubingwa wa mashindano ya Mwalimu Nyerere, baada ya kuichapa Academy Boys 154-152 katika mchezo uliofanyika ndani ya Uwanja wa Chuo Kikuu jijini siku za karibuni.



Hamis Abdallah ambaye ndiye Nahodha wa Academy Boys alisema kwamba amejitahidi kucheza kwa juhudi zote lakini bahati ikaangukia pengine.

Abdallah alisema waliweza kucheza vizuri kadri wawezavyo kwani nia ilikuwa ni kuweza kuutwaa ubingwa huo.

Alimalizia kwa kusema kwamba kuna kushinda na kufungwa na watajitahidi kufanya mazoezi hata yakija mashindano mengin waweze kufanya vizuri zaidi.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.