Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Polisi Bongo yafagiliwa

Jeshi la polisi Tanzania limefagiliwa, kwa juhudi zake kudhibiti na kupambana na wimbi la uhalifu nchini.

Ufagio huo umetolewa Mkuu wa jeshi la polisi kutoka Burundi Inspekta Jenerali Fabian Ndayishimiye ambaye pia ni mwenyekiti wa shirikisho la wakuu wa majeshi ya polisi kwa nchi za maziwa makuu na pembe ya Afrika.

Akiwa katika ziara ya siku tatu Bongo Ndayishimiye amesema Tanzania ni mfano wa kuigwa na nchi nyingine barani Afrika jinsi jeshi hilo linavyopiga mzigo.

Mapema mkuu wa jeshi la polisi nchini inspekta jenerali Said Mwema alisema Tanzania imetekeleza makubaliano yote yaliyofikiwa katika mkutano wa wakuu wa majeshi ya polisi wa nchi hizi mbili.




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.