Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Stars kuanza kuvaana na Kenya

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeamua kufanya mabadiliko ya timu katika makundi ya hatua za awali za michuano mipya ya Afrika, itakayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani.



Katika michuano hiyo mipya ya Afrika kwa Tanzania, timu ya Taifa Stars itavaana na Kenya badala ya Uganda.

Stars ilikuwa ikwaane na Uganda katika mechi ya kwanza lakini sasa itacheza na Kenya, Harambee Stars, ambapo mechi ya kwanza itapigwa nchini Kenya kati ya Machi 28 na 30 kabla ya kurudiana hapa nyumbani wiki mbili baadaye.

Kwani Stars itacheza na Kenya ambako mechi ya kwanza itachezwa Kenya kati ya Machi 28-30 kabla ya kurudiana majuma mawili baadaye hapa nchini.

Kama Stars itafanikiwa kuitoa Kenya, itakutana na mshindi kati ya Uganda na Eritrea, huku mchezo wa kwanza ukifanyika Tanzania kati ya Mei 2 na 4 na mechi ya marudiano kupigwa wiki mbili baadaye.


Pia katika michuano hiyo jumla ya nchi saba zitafuzu na kuweza kuungana na nchi mwenyeji Ivory Cost, kucheza fainali hizo za kwanza Afrika kwa kushirikisha vigogo wanane, na lengo la CAF likiwa ni kuinua vipaji vya wachezaji wanaocheza ndani ya Afrika.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.