Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Ukware kwa madenti wamponza mwalimu.

Mwalimu wa Shule ya Sekondari Milala wilayani Mpanda mkoani Rukwa, Bw. Pascal Isengelo, amelazwa katika hospitali ya wilaya hiyo baada ya kupata kichapo na kujeruhiwa vibaya na wanafunzi kwa tuhuma za imani za kishirikina.

Wanafunzi hao wa kike wa shule hiyo wamedai kuwa kwa muda
mrefu mwalimu huyo amekuwa akiwatokea na akiwaingilia kimwili nyakati za usiku kwa kuwabaka.

Mwalimu akipewa disipilini na madenti hao saa mbili usiku wakati huyo alipoenda shuleni hapo kwa lengo la kukagua wanafunzi kama wamefika katika masomo ya jioni.

Akizungumza na mwandishi katika wodi aliyolazwa, Bw. Pascal alikiri kupigwa na wanafunzi hao.

``Mimi sina tabia hiyo ya kishirikina ambayo wanafunzi hao wanadai bali nadhani ni chuki tu kwa kuwa mimi nafuatilia sana maendeleo yao ya masomo hivyo wananiona kuwa ni mnoko,`` alisema.

Muuguzi Mkuu wa hospitali hiyo, Bw. Pius Buzumale, alikiri kumpokea mwalimu huyo na kuongeza kuwa alifikishwa katika hospitali hiyo akiwa hajitambui baada ya kupoteza fahamu.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.