Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Wivu mwingine hasara tupu.

Jeshi la Polisi mkoani Iringa, linamshikilia mkazi wa kijiji cha Mbugani, Mavanga wilaya ya Ludewa mkoani Iringa Bw. Emmanuel Mwapinga (27), kwa tuhuma za kuiteketeza kwa moto familia yake kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Imedaiwa kuwa mkazi huyo alifanya ukatili huo baada ya kuchukizwa na vitendo vya mkewe na hivyo lengo la kuchoma moto nyumba hiyo lilikuwa ni kuwateketeza watoto wote na mama yao mzazi.

Bw. Mwapinga alikuwa amezaa na mwanamke huyo, Bibi Asunda
Mlelwa (25) mtoto mmoja na baada ya hapo walitengana na kila mmoja alikuwa akiishi kwake.

Hata hivyo, inasemekana sababu kubwa ya Bw. Mwapinga kufikia uamuzi huo ni baada ya kusikia mwanamke huyo anaendeleza urafiki na mwanaume mwingine wa zamani, ambaye alizaa naye mtoto wa miaka minane sasa.

Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Bw. Claus Mwasyeba,aliwaambia wandishi wa habari ofisini kwake, kuwa tukio hilo lilitokea Machi 8 mwaka huu saa 2 usiku.

Bw. Mwasyeba aliwataja watoto waliouawa kwa kuchomwa moto
kuwa ni Edmund Mlelwa (8) na Angelina Mwapinga (2.6).
Hata hivyo, Kamanda Mwasyeba alisema wakati mtuhumiwa huyo
akiteketeza nyumba hiyo kwa moto, mama wa watoto hao hakuwa nyumbani wakati huo alikuwa katika klabu cha pombe akinywa pombe na jamaa zake.

Kwa mujibu wa Kamanda Mwasyeba mtuhumiwa huyo alikuwa
amelenga kuwateketeza kwa moto mama na watoto.

Kaimu Kamanda huyo alisema kuwa mtuhumiwa huyo amekamatwa
na atafikishwa mahakamani wakati wote kuanzia sasa mara tu baada ya upelelezi kukamilika.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.