Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
EPA kunasa mafisadi kibao.

Uchunguzi wa wizi wa mshiko katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) inazidu kunasa sura mpya.

Ikiwa ni siku chache tu baada ya wanaharakati na wanasiasa
kubebea bango kuhoji kuhusu kurejeshwa kwa sehemu ya fedha
zilizoibwa katika akaunti.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, alikuwa kiongozi wa kwanza kuelezea kwa undani kile ambacho timu ya uchunguzi wa kashfa hiyo ambayo yeye ni mjumbe wake .

Akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, IGP Mwema alisema upelelezi wao sasa umekuwa mtambuka,
akionyesha dhahiri kuvuka na pengine kuwagusa watu ambao wako nje ya orodha ya kampuni 22 ambazo ndizo zilizotajwa kuhusika na wizi wa fedha hizo za EPA.

Mwema aliwaambia wahariri hao kuwa, kazi inayofanywa sasa ni kufuatilia mlolongo wa fedha hizo, kutoka zilipoibwa BoT mpaka kwa mtu wa mwisho aliyezipokea.

“Sasa tumeshavuka corporate vein (wigo wa kampuni)…
tunazikusanya fedha bila kujali kwamba ulikwenda benki kuchukua EPA au la. Hili si eneo dogo. Watu wengi wametupa taarifa na sisi hatujadharau hata taarifa moja,” alisema.

Mwema alisema kuwa timu hiyo imelazimika kuchunguza zaidi kwa sababu kama ilivyo katika wizi mwingine, mali ya wizi inaweza kuuzwa kwa mtu zaidi ya mmoja na uchunguzi wa fedha za EPA unaonyesha kuwa mlolongo umekwenda mbali.

Hadi hivi sasa timu ya wataalamu inayochunguza sakata hilo la EPA ilikuwa tayari imefanikiwa kukusanya mbovu zipatazo bilioni 64.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.