Gofu yawaniwa na Sita
Wacheza gofu kadhaa wapendekezwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi Mkuu wa Kamati ya mchezo huo, kwa wanawake ndani ya klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.
Uchaguzi wa viongozi wa kamati hiyo umepangwa kufanyika baadaye mwezi huu klabuni hapo na nafasi sita zitawaniwa.
Nafasi hizo sita mpaka sasa teyari zilishapata wagombea ambao wamependekezwa kuwania uongozi katika uchaguzi huo.
Kwa upande wa nafasi ya nahodha Joyce Svarvar anawania tena baada ya kupendekezwa na atachuana vikali na Lina Nkya.
Naye Stephanie Sayore amependekezwa kuwania tena nafasi ya nahodha msaidizi, lakini safari hii atapambana na Ayne Magombe ambaye alikuwa katibu wa kamati inayomaliza muda wake.
Mbonile Burton, ambaye alikuwa katibu wa mashindano amependekezwa kuwania nafasi ya katibu iliyokuwa ikishikiliwa na Ayne, huku Shazi Mnyombe anawania nafasi ya mhazini iliyokuwa wazi baada ya Nkya kujiuzulu mwaka jana.
Viongozi watakaochaguliwa watakaa madarakani kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kupisha uchaguzi mwingine utakaofanyika mwakani.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala