Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Maisha bora kwa wabongo ndiyo haya?

Wabongo zaidi milioni tano hawana huduma yoyote ya choo, na zaidi ya milioni 20 wapo katika hatari ya kupata magonjwa hatarishi kwa sababu ya kukosa huduma ya choo kilicho safi.

Asilimia hiyo inafanya idadi ya Watanzania wasio na vyoo kuwa zaidi ya milioni 1.7 ikiwa idadi ya Watanzania wote itakuwa milioni 35.

Wakizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es
Salaam,wawakilishi kutoka mashirika mbalimbali ya Umoja wa
Mataifa kuhusu siku hiyo, ambayo mwaka huu inaadhimishwa kama mwaka wa Kimataifa wa Usafi, walisema kuwa hatua hiyo inatoka na serikali kutotilia mkazo katika suala la usafi na afya.

Mshauri wa sera ya usafi kutoka Shirika la Water Aid, Wilhelmina Malima, alisema kuwa kwa upande mwingine, watu wameonekana kutozingatia kanuni za usafi.

Akitoa mfano, alibainisha kuwa asilimia 40 ya watu wanaotoka chooni huwa hawanawi mikono, hali inayowaweka katika hatari ya kuambukizwa magonjwa.

Katika maelezo yake, Malima alisema kuwa uchafu ni matokeo
mabaya ya kuongezeka kwa bakteria ambao husababisha magonjwa ya kuambukiza kama kipindupindu, magonjwa ya tumbo (typhoid) ambayo huua maelfu ya watu kila mwaka na kati yao asilimia 90 ni watoto.

Malima alisema kuwa pesa nyingi zinazotolewa na serikali zimekuwa zikielekezwa kutatua tatizo la maji, lakini si tatizo la usafi, ambalo alilieleza kuwa ni hatari, si tu kwa mtu binafsi, bali pia kwa ukuaji wa uchumi.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.