Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Cheka atamaniwa na Mtambo wa chang'aa

Bondia wa ngumi za kulipwa hapa nchini Maneno Oswald ‘Mtambo wa Gongo’, amewataka waandaaji wa mapambano kujitokeza kumkutanisha yeye na Francis Cheka ili akate ngebe zake.



Maneno alisema kuwa ana uhakika uwezo wa Cheka ni mdogo kwake na anashangazwa na kitendo cha bondia huyo kutoka Morogoro kumpiga Hassan Matumla.

Mmasumbwi huyo alijinadi kuwa uwezo aliokuwanao kwa sasa unatokana na mazoezi ya nguvu, anayoyafanya na yanazidi kumpa uhakika wa kumtwanga Cheka katika raundi za mwanzoni na kurudi kwao Morogoro ili akaendeleze biashara yake ya chupa.

Mbali ya kumtaka Cheka bondia huyo anatarajiwa kuondoka nchini mwishoni mwa Machi kwenda Denmark, atakakozipiga na Fawaz Nazir wa nchini humo.

Alisema pambano hilo litakuwa si la ubingwa bali litafanyika jijini Copenhagen.

Aliwatata mashabiki wake na Watanzania kwa ujumla kutegemea ushindi wa kishindo, kutokana na maandalizi aliyoyafanya.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.