Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Mkwara wa wafanyakazi TRL walipa.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Reli nchini (TRL), wamesitisha mgomo wao baada ya mwajiri wao kukubaliana kimsingi kutekeleza madai yao ya nyongeza ya mishahara.

Makubaliano hayo yalifikiwa na kutangazwa kwa waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika katika ofisi za Wizara Miundombinu.

Majadiliano hayo yaliwahusisha wafanyakazi hao waliowakilishwa na chama chao - TRAWU, serikali kupitia Wizara ya Miundombinu pamoja na mwajiri.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa utiaji saini
makubaliano hayo, Chambo alisema kuwa uongozi wa TRL
umekubali kupandisha kima cha chini cha mshahara kutoka sh
87,000 za sasa hadi sh 160,000 kwa mwezi.

Alisema kuwa mshahara huo utalipwa hadi mwezi Agosti, ambapo mwajiri amekubali kupandisha tena mshahara huo na kufikia sh 200,000, sawa na kiwango ambacho kimetangazwa na serikali.

Makubaliano hayo yalifikiwa baada ya mgomo wa wafanyakazi hao uliodumu kwa siku mbili, wakishinikiza kima cha chini cha mshahara kiongezwe hadi sh 250,000.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.