Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Trafiki wapenda mshiko kubanwa.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, James Kombe,amesema kuwa Jeshi la Polisi limepanga mkakati maalumu ili kuwanasa askari wa kikosi hicho wanaojihusisha na vitendo vya rushwa barabarani, sambamba na unyanyasaji wa madereva na abiria.

Kombe alisema mkakati huo ndio utakaoweza kufanikisha
kuwamwaga kazini askari wote wanaojihusisha na vitendo vya
rushwa.

Alisema mkakati huo umebuniwa baada ya kudhihirika kuwa rushwa imekuwa ikilichafua jeshi hilo kupitia kikosi hicho kama ambavyo malalamiko mbalimbali ya wadau yanavyoonyesha.

Alisema ili kuweza kuwabaini askari hao, watu maaalumu, wakiwamo askari kanzu, watakuwa wakisafiri kwenye mabasi ya abiria ili wajionee wenyewe jinsi askari hao wanavyopokea rushwa na watapaswa kurudisha taarifa kwa viongozi wa juu wa jeshi hilo ili hatua zichukuliwe.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.