Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
BoT yajivua EPA

Benki Kuu ya Tanzania (BoT), imetangaza rasmi
mpango wa kujitoa katika usimamizi wa malipo
katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ambayo
imekumbwa na matatizo ya ufisadi.

Mpango huo umetangazwa jijini Dar es Salaam na
Gavana wa BoT Profesa Benno Ndulu, ambaye pia
ametangaza kujivua uenyekiti na ujumbe wa
Kamati ya Usimamizi wa Hesabu ya benki hiyo,
benki hiyo.

EPA ambayo ni akaunti iliyoanzishwa chini ya
Mfumo wa Ujamaa kipindi ambacho nchi
ilikabiliwa na uhaba wa bidhaa na fedha za kigeni,
awali ilikuwa iko chini ya iliyokuwa Benki ya Taifa
ya Biashara (NBC) kisha ikahamishiwa BoT hadi
sasa.


Akitangaza maamuzi hayo, Profesa Ndulu alisema
lengo la BoT ni kubaki na majukumu yake ambayo
yameainishwa katika Sheria ya Benki Kuu ya
mwaka 2006.

Sheria ya BoT mwaka 2006 pamoja na mambo
mengine, inataja majukumu ya BoT kuwa ni
kusimamia Ukuaji wa Sekta ya Fedha, Uchumi wa
nchi na Usalama wa Mabenki.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.