Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Padri Kimaro atinga uraiani.

Padre Sixtus Kimaro (40), aliyekuwa amekula
mvua ya miaka 35 mwaka 2005 baada ya
kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana
mwenye umri wa miaka 17, ameachiwa huru .

Padri hiyo amechomoka gerezani baada ya
Mahakama Kuu kutupilia mbali hatia zote mbili
na kifungo.

Akitoa uamuzi huo Jaji wa Mahakama Kuu,
Robert Makaramba alisema amemwachia huru
Padri Kimaro kwa kuwa upande wa Mashitaka
haukutoa ushahidi wa uhakika kwa mashtaka
anayodaiwa kuyatenda kwa kijana aliyekamatwa
akiwa naye katika eneo la Changanyikeni, Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam.

Pia Jaji Makaramba alifuta amri ya awali
iliyotolewa ya Mahakama iliyomtaka Padri huyo
alipe faini ya Sh milioni mbili.

Jaji Makaramba alitupilia mbali hatia aliyokutwa
nayo ya ulawiti akisema hakukuwa na ushahidi wa
moja kwa moja unaoonyesha kwamba wawili hao
walikuwa wakitenda jambo lililodaiwa kutendeka.

Baada ya kutolewa uamuzi huo Padri Kimaro
alinyanyua mikono yake juu na macho ikiwa ni
ishara ya kumshukuru mungu kwa hatua
iliyofikiwa na mahakama.

Padre Kimaro alionekana kububujikwa machozi
wakati Jaji akiwa amefikia katikati kusoma
hukumu hali iliyomfanya atumie kitambaa
kujifuta.

Awali akiwasilisha ushahidi wa mteja wake,
Wakili wa Padri Kimaro alisema upande wa
mashitaka ulishindwa kuwasilisha ushahidi wa
kuridhisha kumuunganisha na makosa aliyodaiwa
kukutwa nayo.

Padri huyo alihukumiwa kifungo hicho katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya
kupatikana na hatia katika mashitaka yote
matatu yaliyokuwa yakimkabili ya kulawiti,
shambulio la aibu na kumdhalilisha mvulana
huyo.

Alihukumiwa kifungo cha miaka 30 jela katika
kosa la kwanza la kulawiti na miaka mitano katika
kosa la pili la shambulio la aibu na kumtaka
mshitakiwa huyo kumlipa Sh2 milioni mvulana
aliyelawitiwa. Adhabu hizo zilikwenda sambamba.

Source:Mwananchi.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.