Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Kwanza lazima kanuni kuzingatiwa

Mwenyeketi wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) Iddi Kipingu amewaasa waandaaji wa mashindano ya Vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Copa Coca Cola kwa kuzingatia kanuni ili kufanya mashindano yawe katika hali ya ubora zaidi.



Kipingu alisema suala muhimu la kuzingatia ni umri wa wachezaji na nilazima waandaaji waweke msimamo wa pamoja kwa kuhakikisha kanuni hazipindishwi.

Alisisitiza kwamba timu zinatakiwa kuwekeza kwa wachezaji wadogo kwani ni chimbuko la maendeleo ya soka ndani ya nchi na hata nje ya nchi pia.

Kwani mashindano ya mwaka huu yanatarajia kuchipua mwezi ujao katika ngazi ya Wilaya, na fainali zake zitakuwa katika ngazi ya Taifa na zikitarajia kufanyika Juni mwaka huu.

Pia baada ya hitimisho la mashindano hayo kitachaguliwa kikosi cha wachezaji bora, kitakachofanya ziara ya mafunzo nchini Brazil.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.