Vifaa vya Judo vyakwama Bandarini
Vile vifaa vya mchezo wa Judo vilivyoletwa nchini kwa msaada wa Shirikisho la judo la Ulaya (EJU), vimekwama bandarini kutokana na kushindwa kukombolewa na Chama cha judo Tanzania ( JATA).
Naye Katibu Mkuu wa JATA Shaaban Kashinde alisema vifaa hivyo viliwasili nchini mwezi Novemba hapo mwaka jana.
Katibu huyo alisema sababu za kukwama kwa vifaa hivyo yakiwemo Magodoro 144 yenye thamani ya dola za Kimarekani 810, ni kutokana na kushindwa kulipia ushuru unaofikia kiasi cha shilingi milioni tano.
JATA iliweza kuwasilisha barua ya maombi ya msaada na BMT, kwani walihaidiwa kusaidiwa vifaa hivyo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala