Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Serikali ya mseto yaja Zenji.

Chama cha Wananchi (CUF) kimesema kimekubaliana
na CCM kuwapo kwa mfumo wa kugawana madaraka
ambao utekelezaji wake utaanza mara baada ya Muafaka
kutiwa saini.

Akizungumza jana na umati mkubwa wa wafuasi wa CUF
katika uwanja wa Kibanda Maiti , Katibu Mkuu wa CUF,
Maalim Seif Sharif Hamad, alisema chama chake
kitaingia madarakani muda mfupi mara baada ya kutiwa
saini makubaliano hayo.

Mkutano huo ulikuwa maalumu kwa ajili ya kutoa taarifa
kuhusu mazungumzo ya Muafaka kati ya CUF na CCM
ambapo kwa sasa yamefikia tamati.

Maalim Seif ambaye alikuwa mgombea urais katika
uchaguzi mara tatu katika mfumo wa vyama vingi kuanzia
mwaka 1995, alisema chama chake kimeridhia
makubaliano hayo yote na kuamua kuyaleta kwa
wananchi.

Alisema kwa sasa kazi iko kwa CCM ambao wanatakiwa
nao kuridhia makubaliano hayo na kuyapeleka kwa
wanachama wake.

Maalim Seif alisema yeye yuko tayari kufanya kazi katika
Serikali yoyote kwa maslahi na manufaa ya wananchi wa
visiwa vya Unguja na Pemba.

Mazungumzo ya Muafaka kati ya vyama vya CCM na
CUF yalichukua karibu miezi 28 ambapo jumla ya mada
kuu nne zilizungumzwa.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.