Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Watakiwa kutosoma.

Katika hali isiyokuwa ya kawaida,waumini watatu wa
Kanisa la Waadventista Asilia, wamehukumiwa kifungo
cha miaka miwili jela, baada ya kupatikana na hatia ya
kuwazuia watoto wao kusoma.

Hukumu hiyo ilitolewa katika Mahakama ya Wilaya ya
Bunda na Hakimu Richard Maganga kwa madai kuwa
Yesu anakuja.

Waliohukumiwa kifungo hicho ni Amos Lutara (40), mkazi
wa Kiagata Wilaya ya Musoma Vijijini, Joyce Paulo (41)
na Nyanjura Machumu (35), wakazi wa Bunda mjini.

Hakimu Maganga alitoa hukumu hiyo baada ya
washitakiwa hao kukiri kosa hilo na kusema kuwa
hawaoni umuhimu wa watoto hao kusoma kwa kuwa
mwisho wa dunia umefika.

Awali, Mwendesha Mashitaka, Mkaguzi Msaidizi wa
Polisi, Edward Manoni, alidai washitakiwa hao walitenda
kosa hilo Machi 10, mwaka huu.

Alidai waumini hao waliwachukua wanafunzi hao na
kuwapeleka katika Kijiji cha Kiagata kwa madai kuwa
waende kumsubiri Yesu anayetarajiwa kuja mwezi ujao
kwa sababu Kijiji cha Kiagata ndicho kilichobarikiwa.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.