Zitto, Slaa waula bungeni
Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekutana Dar es Salaam kuchagua wenyeviti wa kamati mpya za Bunge ambapo wabunge machachari wa kambi ya upinzani na chama tawala, wameibuka washindi katika kamati nyeti.
Wabunge walioibuka na ushindi katika uchaguzi huo ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini Bw. Zitto Kabwe (CHADEMA) ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati mpya ya Hesabu za Mashirika ya Umma.
Wengine ni Mbunge wa Karatu, Dkt. Wilbroad Slaa (CHADEMA),
ambaye tofauti na wagombea wa kamati nyingine ambao walikuwa na wapinzani, alipita bila kupingwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa .
Kwa upande wa Kamati ya Hesabu za Serikali, Mbunge wa Bariadi Mashariki, Bw. John Cheyo (UDP), amechaguliwa kuendelea na wadhifa wake wa uenyekiti ambapo Makamu wake alichaguliwa kuwa Mbunge wa Kwamtipura, Bw. Zubeir Ali Maulid (CCM).
Aidha, Mbunge wa Same Mashariki, Bibi Anne Malecela (CCM),
alichaguliwa kuongoza kamati mbili; Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, ambako alichaguliwa kuwa Mwenyekiti na Kamati ya Miundombinu kuwa Makamu Mwenyekiti.
Katika Kamati ya Haki na Maadili na Madaraka ya Bunge, Bibi Malecela atasaidiwa na Mbunge wa Mafia, Bw. Abdulkarim Shah

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala