Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Je nitapata wapi beki wa kulia?

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Marcio Maximo, sasa yupo kwenye mikakati ya kutafuta mrithi wa beki wa kulia wa kikosi hicho.



Kocha huyo amelazimika kumtema mchezaji huyo Nassor Said ‘Cholo’, kutokana na majeraha aliyokuwanayo.

Maximo alisema amepokea taarifa kutoka kwa uongozi wa klabu ya Simba kuwa, Cholo anasumbuliwa na majereha ya mguu alioumia hivi karibuni na anaendelea na matibabu Hospitali ya Aga Khan.

Cholo kwa sasa ameweza kupewa wiki mbili za mapumziko bila kujihusisha na shughuli za soka.

Maximo alisema kuwa hivi sasa yuko kwenye mikakati ya mwisho ya kumteua mchezaji atakayemudu vema nafasi ya beki wa kulia, ambayo ni ngumu na kesho kutwa anatarajia kumtangaza.

Alisema namba hiyo ilikuwa na wachezaji wawili aliowateua kwenye kikosi hicho kinachojiwinda na mechi ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Msumbiji ‘Black Mambaz’, ambao ni Cholo pamoja na beki kutoka mabingwa wa Zanzibar, Miembeni, Salumu Juma.

Kocha huyo aliongeza kuwa analazimika kuongeza mchezaji mwingine ikiwa ni tahadhari, endapo itatokea beki huyo aliyesalia akapatwa na majeraha.

Alisema ailikuwa anamtegemea sana Shadrack Nsajigwa kwani naye ana adhabu kwenye klabu yake, pia alimuongeza Said Sued na yeye ni majeruhi.

Kutokana na wachezaji hao kuwa hivyo akaona amuongeze Nassor Said, ambaye na yeye amepata majeraha.

Kocha huyo amekumbwa na wakati mgumu sana juu ya kumpata mchezaji anayeweza kuwafikia hawa aliowachagua.

Stars inajiwinda na michuano ya awali ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika, kwa wachezaji wanaocheza ligi za nyumbani zitakazofanyika Ivory Coast mwakani ambako itaanza kampeni yake kwa kucheza na Kenya Machi 30.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.