Kichanga kilichozikwa,chazikwa tena
Katika hali inayotafsiriwa kuwa uzembe wa watumishi wa Afya,kichanga cha kiume kilichokufa baada ya kuzaliwa, kimezikwa mara mbili na wanafamilia mbili tofauti, mkoani Shinyanga.
Hali hiyo imetokana na mfanano wa majina ya wazazi wa wawili hao waliokwenda kujifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya mkoa huo kutoka vijiji tofauti na kubadilishiwa watoto.
Akizungumzia tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Charles Nyanda, alisema utata huo ulitokea Machi 14 mwaka huu.
Kamanda huyo aliwataja wanawake waliokumbwa na mkasa huo
kuwa ni Chiristina Budeba (30), mkazi wa Kijiji cha Busangwa na Chiristina Bundala (28) kutoka Kijiji cha Bugogo, wilayani Shinyanga Vijijini waliojifungua watoto wa kiume kila mmoja.
Alisema, Budeba alijifungua mtoto akiwa hai wakati Bundala, alijifungua mtoto mfu na wote walihudumiwa na wahudumu tofauti wa chumba cha upasuaji.
Baada ya muda, mume wa Budeba aliyejulikana kwa jina la Masaliga Lutaja, ambaye mkewe alijifungua mtoto akiwa hai alipofika katika hospitali hiyo ili kujua hali ya mke wake, wauguzi wa zamu siku hiyo walimpa pole na kumfahamisha kuwa mtoto aliyezaliwa kwa upasuaji,
amekufa.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala