Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Dawasco kimbembe na bosi wao.

Wafanyakazi wa Shirika la Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASCO), wamemkataa Mkurugenzi Mkuu
wao, Bw. Alex Kaaya, wakimtaka aachie ngazi kwa madai
kuwa ameshindwa kutimiza ahadi za wafanyakazi wake.

Mbali ya kumtaka Bw. Kaaya ajiuzulu, wafanyakazi hao
pia wamesema kutokana na mfumo mbaya wa
uendeshaji wa DAWASCO unaosababishwa na
menejementi, ni bora shirika hilo likavunjwa badala ya
kuendelea kuonekana lipo wakati uongozi umeshindwa
kufanya kazi.

Wakizungumza Dar es Salaam katika mkutano maalumu
uliotishwa na wafanyakazi wa DAWASCO kwa lengo la
kutoa kero zao, walidai kuwa Bw. Kaaya na viongozi wa
ngazi mbalimbali ndio waliosababisha shirika hilo lifike
lilipo katika hatua ya kushindwa kutoa huduma bora kwa
wananchi.

walisema Bw. Kaaya amewagawa
wafanyakazi kwa kiasi kikubwa na kufikia hatua ya baadhi
yao kutoelewana na kuwapo kwa mpasuko ambao
unarudisha nyuma maendeleo ya shirika na matokeo
yake ni kero za kila aina.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.