Serikali kutoendelea kula bati .
Serikali imesikia kilio cha wanafunzi wa vyuo vikuu baada
ya kutangaza kuongeza posho kwa ajli ya mafunzo kwa
vitendo kutoka Sh 6,000 zinazodaiwa kuwa hazitoshi hadi
Sh 10,000 kwa siku.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne
Maghembe aliyasema hayo alipozungumza na Jumuiya
ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam cha Mkwawa Iringa.
Alisema mbovu hizo zitaanza kutolewa kwa wanafunzi
hao kuanzia mwaka ujao wa fedha kwa kuwa
zimeshaingizwa katika makadirio ya bajeti ya wizara hiyo.
Mbali ya kuongeza mshiko huo serikali itaanza kutoa
mikopo kwa wahadhiri wasaidizi ili wajiendeleze
kitaaluma.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala