Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Mkwasa kuipiga msasa Miembeni

Yule Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Wanawake Tanzania ‘Twiga Stars’, jana alisaini rasmi mkataba wa kuwanoa mabingwa wa soka visiwani hapa Miembeni, ‘Chelsea ya Zenji’.



Naye Mkurugenzi wa Miembeni Amani Makungu alisema mkataba na kocha huyo utakuwa wa miezi mitatu.

Makungu alisema mambo yote wamekamilishiana na kocha huyo ikiwamo posho zake, nyumba pamoja na usafiri.

Alisema jukumu la Mkwasa ni kuinoa Miembeni kwa ajili ya Ligi Kuu ya Zanzibar inayoendelea na michuano ya Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki, maarufu kama ‘Kagame Cup’.

Makungu aliongeza kuwa, wana imani na Mkwasa kuwa ataifanyia makuu Miembeni, na kama mambo yatakuwa mazuri wanaweza kuongeza mkataba huo na Mkwasa.

Mkwasa alisema, ameweza kufarijika baada ya kupata nafasi ya kufanya kazi katika visiwa hivyo, hususan kuinoa Miembeni.

Alisema kwamba atajitahidi kuipa mafanikio timu hiyo wakati wa kuinoa, na aliweza kuondoka hapo kisiwani na kuelekea Pemba kwa kuanza kukabiliana na majukumu yake mapya.

Mbali ya kuwa Kocha Mkuu wa Twiga Stars amewahi kuzinoa timu kadhaa, zikiwamo Prisons ya Mbeya, Yanga, Moro United na nyinginezo.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.