Nishati na madini kimbembe na wabunge..
Wizara ya Nishati na Madini, inaingia katika mtihani mwingine wa kutaka huruma za wabunge wakubali kuupitisha muswada wa petroli nchini, kabla ya kuwasilishwa katika kikao cha Bunge la kinachotarajiwa kufanyika mwezi ujao mjini Dom.
Hivi karibuni wabunge hao wamekuwa msumari kwa serikali
kutokana na kutamka wazi kuwa, hawapo tayari kuwa chambo kwa kutumika kama mihuri ya kupitishia miswada kwa maslahi ya wachache.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, wabunge hao, walikataa kwa mara ya pili kupitisha muswada wa sheria ya umeme katika semina iliyokuwa na lengo la kuwaelimisha umuhimu wa kuwapo kwa sheria hiyo.
Leo wanatarajia kuendelea na semina ya mafunzo kuhusu ya
muswada wa petroli itakayofanyika jijini Dar es Salaam, ambayo pamoja na mambo mengine, wakati serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli (TPDC), imeamua kuanzisha akiba ya mafuta nchini.
Tayari wabunge hao wametamka kuwa, hawana imani na wizara
hiyo, iliyokuwa ikiongozwa na Nazir Karamagi ambaye alijiuzulu uwaziri hivi karibuni baada ya kuhusishwa na kashfa ya Mkataba wa Kampuni ya kufua umeme ya Richmond ya Marekani.
Mambo yanaonekana bado si shwari kwani pamoja na Karamagi
kuondoka, bado mzimu wake, umekuwa ukitawala, kufuatia wabunge kusisitiza miswada hiyo ni ile ile tena akiwa ameisaini.
Tayari wabunge hao wamegawiwa miswada hiyo wiki iliyopita,
ukiwamo ule wa petroli na umeme, lakini wameikosoa, wakisema haina jipya wala maslahi kwa wananchi.
Wabunge hao, waliongeza kusema kuwa, wamechoshwa na tabia ya serikali kuwapa vitu muhimu vinavyohusu maslahi ya nchi kwa muda mfupi, kabla ya kuingia katika vikao au semina, kwa lengo la kujadiliwa huku ikiwalipa posho ya Sh 80,000 kama njia ya kuwapumbaza ili wapitishe.
Semina hiyo ya leo ni muendelezo wa semina ya kujadili muswada wa umeme na petroli iliyovunjika katika Kikao cha Tisa cha Bunge, baada ya Wabunge hao kususia mpaka wapatiwe ripoti ya uchunguzi ya kamati Teule ya Bunge, iliyoundwa kuchunguza mchakato wa zabuni iliyoipa ushindi kampuni ya Richmond .

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala