Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
'Wazungu wa unga Zenj ni nyomi'

Wafanyabiashara wanaoingiza madawa ya kulevya Zenj
wanafahamika na wanaongezeka kwa kasi, na kwamba imefika
wakati serikali kutoendelea kuwalia bati.

Hayo yamesemwa Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Zanzibar, Augustine Ndelikiyama Shao.

Amesema wakati umefika kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na ile ya Tanzania zitangaze kuwa tatizo la madawa ya kulevya ni janga la kitaifa.

“Naamini kwamba wadau wa biashara hizi wanafahamika na kwa
uhakika serikali na vyombo vyake wakitaka, wanaweza kulimaliza tatizo hili.

Alisema hayo wakati wa ibada ya Jumatatu ya Pasaka iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Minara miwili, Mtaa wa Shangani, Mji Mkongwe wa Zanzibar.

Aliwaeleza waumini kwamba, idadi ya wasambazaji na watumiaji wa madawa hayo imeongezeka kwa asilimia 24, hali ambayo inavilazimisha vyombo vinavyohusika kuchukua hatua za ziada kukabiliana na tatizo hilo.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.