Michuano ya Darts kuchekecha Kampala
Hatimaye lile Shirikisho la Mchezo wa Darts kwa Nchi za Afrika Mashariki, limeandaa michuano ya sita ya ubingwa utakaofanyika mwakani ndani ya jiji la Kampala.
Mwenyekiti wa Chama cha Ridhaa cha Darts Tanzania Gesase Waigame alisema hatua hiyo imefikiwa wakati wa fainali ya michuano ya Tano iliyokuwa ikifanyika kwenye Ukumbi wa Kirumba Resort, jijini hapo.
Waigame alisema shirikisho hilo limepitisha kuwa michuano ya wazi ya mchezo wa Darts kwa nchi wanachama yatafanyika Septemba mwaka huu.
Uganda imeibuka na ubingwa katika michezo iliyokutanisha nchi kwa nchi, na kuwavua mabingwa watetezi Kenya walionyakua ubingwa huo mwaka jana.
Alisema kutokana na ushindi huo Uganda walikabidhiwa kombe pamoja na kitita cha Sh 140,000 huku Tanzania ambayo iliibuka mshindi wa pili ilijisombea Sh 70,000.
Klabu ya APTC ya Kenya ilijitwalia ubingwa kwa upande wa klabu na klabu na kujizolea Sh 140,000, wakati Chuo cha Waganga cha Mulago kutoka Uganda chenye klabu mbili za wachezaji wa fani ya upasuaji na ile ya macho kila moja ilizawadiwa Sh 40,000 baada ya kushika nafasi ya pili.
Mwenyekiti wa Chama hicho cha Riadha alisema kwamba wachezaji 60 wa hapa nchini waliojitokeza kushiriki michuano hiyo, kwani hawakuweza kufanya vizuri kama ilivyotarajiwa kutokana na ukata.
Alisema kwamba wachezaji hao walishindwa kujiandaa vizuri kutokana na uhaba wa kifedha.
Aidha alimalizia kwa kutoa wito kwa serikali, mashirika, makampuni pamoja na wadau wa michezo nchini kujitokeza kwa wingi ili

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala