Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
MP,s wapitisha muswada wa petroli.

Wabunge wameridhia muswada wa kuanzishwa sheria mpya ya
biashara ya mafuta ya petroli na kuitaka serikali kuimarisha Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), ili liweze kuagiza na kuuza petroli.

MP,s hao walisema mabadiliko ya sera yaliyofanywa na serikali miaka michache iliyopita ya kutoipa madaraka ya kuagiza na kuuza mafuta TPDC yalifanyika kimakosa na yamelisababishia taifa hasara kubwa sambamba na kuongeza bei ya mafuta ya petroli.

Hayo waliyabainisha kwenye semina ya kujadili miswada ya sheria mpya za biashara za mafuta ya petroli, inayotarajiwa kuwasilishwa bungeni mwezi ujao, iliyoandaliwa na Wizara ya Nishati na Madini.

Mbunge wa Wawi, Hamad Mohamed Rashid (CUF), alisema serikali inapaswa kuachana na dhana kuwa taasisi za umma haziwezi kufanya biashara, bali kinachotakiwa hivi sasa ni kuziwezesha, ili ziweze kufanya biashara husika.

Mbunge wa Lindi, Suleiman Kumchaya, alisema muswada huo
umeweka adhabu ndogo ya faini ya sh milioni 10 na kifungo cha miaka 5-7 kwa watu wanaochanganya mafuta ya taa na petroli na kutaka adhabu iongezewe zaidi kwa wahusika kufilisiwa mali zao na kutumikia kifungo kuanzia miaka 10-15.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Yona Kilaghane, alisema
wanahitaji mbovu zipatazo dola milioni 30 kwa ajili ya kujijengea uwezo na kushiriki katika miradi mbalimbali.

Alisema fedha wanazohitaji hivi sasa watazitumia katika kusambaza gesi ya asilia katika nyumba zipatazo 30,000 na magari yapatayo 8,000 hivyo TPDC kuwa moja ya vyanzo vya kuliletea taifa fedha.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema michango ya wabunge hao imewasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha miswada ya sheria mpya za umeme na biashara za mafuta ya petroli.

Miswada ya sheria mpya za umeme na biashara za mafuta ya petroli ilizua tafrani zaidi wiki iliyopita pale wabunge walipogomea muswada wa umeme wakidai una lengo la kuliua Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania na kuwabeba wawekezaji.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.