Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Naisifu Tanzania

Hatimaye Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imetoa pongezi kwa Tanzania na wananchi wake, kwa ushirikiano mkubwa waliouonyesha wakati wa mbio za Mwenge wa Olimpiki zilizofanyika hapa nyumbani siku za karibuni.



Naye Balozi wa China nchini Tanzania Liu Xinsheng alitoa pongezi hizo wakati akikabidhi mchango wa vifaa vyenye thamani ya dola za Kimarekani 3,200 (zaidi ya Sh milioni 32) kwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo George Mkuchika wa hapa mjini.

Balozi huyo aliweza kuusifu ushirikiano wa miaka mingi baina ya serikali hizo mbili, ambao umekuwa ukiimarika siku hadi siku katika nyanja mbalimbali za kimaendeleo.

Pia ameishukuru Tanzania kwa kuiunga mkono China katika harakati zake za kufanikisha uenyeji wa michuano ya Olimpiki, itakayofanyika Beijing, Agosti mwaka huu.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.