Judo Z`bar kufanyika Juni na Julai
Chama cha Judo Zanzibar (ZJA) kimeandaa mashindano ya kitaifa ya mchezo huo, yanayotarajiwa kufanyika kati ya Juni na Julai.
Kocha mkuu wa mchezo huo Tsyushi Shimaoka alisema mashindano hayo yamepangwa kufanyika kwenye ukumbi wa Budokan Amaan, mjini Unguja.
Shimaoka alisema lengo la mashindano hayo ni kuweza kuteua timu ya taifa, na yatashirikisha wachezaji kutoka pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Bara na Zanzibar.
Alisema wachezaji wanaotakiwa kushindana ni wale wenye uzito kati ya kilo 60 na 100.
Kocha huyo alisema kwamba wanatarajia kupata wachezaji wazuri baada ya mashindano hayo, na watakao weza kuiwakilisha vyema Tanzania katika michuano ijayo ya Afrika Mashariki na Kati.
Pia chama hicho kinatarajia kuanzisha rasmi mchezo huo kisiwani Pemba, kuanzia mwezi Agosti kwa lengo la kuuinua vipaji ndani ya visiwani hivyo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala