Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Safari ya gofu Zambia yaota nyasi

Hatimaye Timu ya Taifa ya mchezo wa gofu ya Tanzania haitashiriki tena mashindano ya Kanda ya Sita, yaliyopangwa kuanza Aprili 23 mjini Lusaka, Zambia.



Naye Kocha Mkuu wa timu hiyo Charles Farrar alisema timu hiyo ilikuwa itimke nchini Aprili 21 kuelekea Zambia, kutokana na kukosa kiasi cha sh. milioni 12 kumeifanya isishiriki mashindano hayo.

Kwa kweli ni aibu kwa timu ya Taifa ya gofu kutoshiriki michuano kama hiyo, na hali kushiriki mashindano hayo ilikuwa ikijulikana tangu mwaka jana.

Alisema kutokana na kukosa michuano hiyo wameamua kuelekeza nguvu katika mashindano mengine ya Afrika Mashariki na Kati yanayorajia kuanza Novemba nchini Kenya.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.