Kikapu yapigwa kalenda
Ile Ligi ya Muungano ya mchezo wa mpira wa kikapu iliyopangwa kuanza Aprili 26 Zanzibar, imesogezwa mbele kutokana na maandalizi yake kutokamilika.
Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kikapu Tanzania (TBF) Lawrence Cheyo, alisema kuwa ligi hiyo haitafanyika tena kama ilivyopangwa kutokana na wenyeji kutokamilisha maandalizi.
Alisema wenyeji wao hawajakamilisha ligi yao ambayo hutoa timu nane (nne za wanaume na wanawake), ambazo zitachuana na wapinzani wao kutoka Bara ili kupata bingwa wa Muungano.
Katibu huyo aliongeza kwamba kutokana sababu hiyo michuano hiyo imesogezwa mbele na sasa itafanyika Mei 17 hadi 23 Zanzibar, na itashirikisha jumla ya timu 16.
Timu hizo zikiwemo za Tanzania Bara ambazo zitashiriki kwenye michuano hiyo, na kwa upande wa wanaume ni Savio, ABC, Arusha Kings na Dodoma Spurs wakati kwa upande wa wanawake ni ABC, Lady Lion, Cargo Ladies na CMTU.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala