Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Viongozi wa netiboli kusheheni kwenye semina

Hatimaye ile semina ya tano ya makocha wakiwemo na waamuzi wa mpira wa Netiboli kutoka nchi za Afrika Mashariki, inatarajiwa kuanza leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa hapa nyumbani.



Anna Bayi ambaye ndiye Mwenyekiti wa Chama cha Netiboli Tanzania (Chaneta), alisema semina hiyo itaongozwa na mkufunzi wa kimataifa wa mchezo huo kutoka Uingereza, Liz Broomdhead aliyewasili nchi ni jana.

Mwenyekiti huyo alisema kwamba semina hiyo itaanza leo na kutarajiwa kumalizika Jumamosi ijayo, na itashirikisha nchi za Kenya, Uganda, Burundi, Zanzibar wakiwemo na wenyeji wa hapa nyumbani Tanzania.

Bayi alisema anaimani kwa asilimia mia moja kuwa semina hiyo itawawezesha makocha na waamuzi wa mchezo huo, jinsi ya kuzielewz vema sheria za mchezo huo ambazo zinatumika kimataifa.

Aliwasisitiza wadau wa netiboli waweze kujichomoza kwa wingi ili kuweza kushiriki semina hiyo, ambayo amaamini itawawezesha wadau wa mchezo huo kujua mengi zaidi kwa undani.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.