Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Lazima Kombe libaki hapa nyumbani

Wilaya ya Kinondoni, Ilala na Temeke za hapa nyumbani zitashiriki kwenye michuano ya Kombe la Taifa kama mikoa tofauti, na zimetakiwa kuunda kamati za ushindi ili kuhakikisha kombe hili linabakia ndani ya jiji la Kandoro.



Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Abbas Kandoro awataka wakuu wa wilaya hizo katika soka, zitambulike kama mikoa ili kuhakikisha wanaunda kamati za ushindi katika timu zao kwa ajili ya kufanikisha maandalizi ya michuano hiyo.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema ameamua iwe hivyo ili kuwezesha kombe hilo lisiondoke ndani ya jiji la Dar es Salaam.

Kandoro alitoa wito huo baada ya kukabidhiwa Sh milioni tatu za maandalizi kwa ajili ya mikoa hiyo.

Pia Mkuu huyo aliwakabidhi Wakuu wa Wilaya hizo tatu Fabian Massawe (Kinondoni), Patrick Tsere (Ilala) na Abdallah Kihato (Temeke), ambao kila mmoja alipokea kwa mbwembwe na kumtambia mwenzake kuwa atalibakisha kombe hilo.

Kandoro aliweza kutoa onyo kwa viongozi wa timu hizo kutochagua wachezaji wenye majina makubwa tu, badala ya kuangalia viwango na uwezo wa wachezaji.

Alisema anawapa tahadhari viongozi hao katika kuchagua timu zao kwani lengo lao, na kulibakisha kombe hilo hapa nyumbani ili waweze kuchagua wachezaji wenye viwango na uwezo na wala siyo kuangalia majina tu.


Michuano ya ‘Safari Lager Taifa Cup’ itakayoshirikisha mikoa 23 ya Tanzania itaanza kutimua vumbi hapa jijini kuanzia Mei 6, na bingwa atajinyakulia kombe zikiwemo na Sh milioni 30 huku mshindi wa pili atapata Sh milioni 15 wakati wa tatu atazawadiwa Sh milioni 7.5.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.