Natarajia kutaja kikosi
Hatimaye Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars Marcio Maximo, anatarajia kutajngaza kikosi kitakachokwaana na Uganda, katika mechi ya kusaka tiketi ya kucheza fainali mpya za Afrika za nyota wa ligi za nyumbani, itakayopigwa nchini Mei 3.
Mechi hiyo ya kwanza itapigwa hapa nchini Mei 3 ndani ya Uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza, kabla ya kurudiana mjini Kampala, Uganda wiki mbili baadaye.
Aprili 28 kikosi cha timu hiyo kitaingia kambini hapa hapa nyumbani kwa nia ya kujinoa kwa mechi hiyo, dhidi ya Waganda kabla ya kwenda jijini Mwanza Mei Mosi ikiwa ni siku mbili kabla ya mechi.
Mechi ya mwisho ya Stars kucheza katika Uwanja huo wa Kirumba ili kuwa mwaka jana, katika kampeni ya kusaka tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Ghana dhidi ya Senegal iliyoisha kwa sare ya 1-1.
Stars ilitinga hatua ya pili kwa kuing’oa Kenya kwa jumla ya mabao 2-1, na inalazimika kushinda mechi hiyo kabla ya mechi ya marudiano itakayopigwa jijini Kampala wiki mbili hapo baadaye.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), kiingilio cha mechi hiyo ya Mei 3, ni sh 20,000 kwa jukwaa kuu na mzunguko itakuwa sh 5,000.
Fainali hizo mpya zenye lengo la kukuza vipaji vya nyota wanaokipiga katika ligi za ndani, zitafanyika kwa mara ya kwanza mwakani nchini Ivory Coast huku nchi shiriki zikiwa zimegawanywa katika kanda sita.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala