Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Hatima yetu kujulikana leo

Hatimaye wachezaji wafuatao Ivo Mapunda pamoja na Shadrack Nsajigwa wa Yanga, wanatarajia kumaliza adhabu yao ya miezi sita.



Naye Katibu Mwenezi wa Yanga Francis Lucas licha ya adhabu ya wachezaji hao kufikia tamati, lakini kurejea kikosini kutaamuliwa.

Wachezaji hao wanatarajiwa kumaliza adhabu yao leo lakini hawataruhusiwa kujiunga na timu, hadi hatima yao itakapoamuliwa na kikao cha Kamati Kuu.

Wachezaji hao walifungiwa kwa utovu wa nidhamu baada ya kutoroka kambini Morogoro, ambako Yanga ilikuwa imepiga kambi kwa madai ya kuhofia usalama wao baada ya Yanga kufungwa na Simba Oktoba 24.

Licha ya kuzuiwa kuondoka pia waliweza kurejea jijini huku timu yao ikikabiliwa na mechi dhidi ya Kagera Sugar, na hivyo wakafungiwa miezi sita.

Adhabu yao ya kifungo cha miezi sita imefikia tamati lakini walielezwa kwamba ni lazima wasubiri hatima yao, itakayoamuliwa na Kamati Kuu itakayokutana leo.

Kufungiwa kwa nyota hao kuliwafanya kuondolewa hata katika kikosi cha timu ya Tanzania Taifa Stars, kilicho chini ya Mbrazili, Marcio Maximo.





 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.