Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
'Wafagilieni mnapokuta waume na ndomu'

Wanawake wametakiwa kutokasirika pindi wanapokuta kondomu
katika mifuko au mabegi ya waume wao na badala yake
wawapongeze kwa kuwa wanaonyesha kujali afya zao na za wenza wao.

Wito huo ulitolewa na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Charles Gishuli, alipokuwa anazindua kampeni ya mapambano dhidi ya ukimwi inayoratibiwa na kampuni T-MARC, katika kampeni ya ‘Sikia kengele, tulia na wako’ iliyofanyika katika viwanja vya mashujaa .

Alisema wanawake wengi wamekuwa na tabia ya kukasirika na
kuzua ugomvi ndani ya nyumba pindi wanapokuta kondomu katika mifuko ya suruali au mikoba ya safari ya waume zao, kitendo ambacho alikemea kwa madai kuwa kinachangia maambukizi mapya ya VVU.

“Unapoona mumeo anajitayarisha kwa safari nenda dukani
kamnunulie kondomu na mfungashie na anaporudi kagua kama
ukikuta zimetumika moja au mbili mpongeze, huyo ni mume makini anayejali afya yako, msikubali kufa kwa sababu ya wivu,” alisema Gishuli.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.