Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Amuua baba yake kwa kisasi.

Jeshi la Polisi Mkoani Singida, linamshikilia mkulima mmoja mkazi wa kijiji cha Damakia,Tarafa ya Ikungi Singida vijijini kwa tuhuma za kumuua baba yake mzazi kwa kumpiga na kitu chenye ncha kali kichwani na kufa papo hapo.

Kisa cha mtuhumiwa kumuua baba yake kikatili ni kutokana na kile kilichosadikiwa marehemu alikuwa akimtolea ushahidi mahakamani ili afungwe kutokana na kesi iliyokuwa ikimkabili.

Kamanda wa Polisi mkoani Singida, Kamishna msaidizi wa Polisi Bi.Celina Kaluba, alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita saa sita mchana na kumtaja mtuhumiwa huyo kuwa ni Bw.Silvery Adriano (40).

Bi. Kaluba alisema mtuhumiwa alimvamia baba yake aliyemtaja kwa jina la Adriano Michael (65) mkazi wa kijiji cha Samaka.

Alisema siku ya tukio, mtuhumiwa alimwona baba yake akiwa katika shuguli zake za shamba umbali wa mita 60 hivi kutoka kwenye nyumba yake ambapo alimfuata kisha kumpiga kichwani kwa kutumia kitu chenye ncha kaliambapo aliaguka na kufa papo hapo.

Aidha Kamanda Kaluba alibainisha kwamba baada ya mtuhumiwa huyo kufanikisha lengo lake la kukatisha maisha ya baba yake mzazi,alimburuza kutoka barabarani hadi umbali wa zaidi ya mita 10 ndani ya shamba la mtama mali ya marehemu kwa nia ya kuficha mwili wake.

Hata hivyo Mwenyekiti wa Kitongoji cha Samaka Bw.Selvester Salvii, alisikia kelele kutoka eneo la tukio na alipofuatilia, alimkuta mtuhumiwa akiwa amesimama kando ya mwili wa baba yake ambaye kwa wakati huo alikuwa tayari amekufa.

Mwenyekiti huyo alipiga yowe na wanakijiji walikusanyika katika eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha kituo kidogo cha Polisi Ikungi.

Bi. Kaluba, alisema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha mauaji hayo ambayo yanaonesha dhahiri ni ya kulipiza kisasi, ni marehemu kutoa ushahidi katika Mahakama ya Mwanzo Ikungi, uliolenga kumtia hatiani mwanawe huyo.

Alisema kuwa mtuhumiwa alikuwa anakabiliwa na kesi ya kutishia kuua kwa maneno na marehemu alitoa ushahidi dhidi ya mwanawe katika mahakama hiyo yapata siku nne zilizopita.



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.