Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Stars kukosa chansi-Tenga

Hatimaye lile Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) latamka kwamba wachezaji wa timu ya Taifa Taifa Stars, hawataruhusiwi kucheza shindano la Kombe la Taifa linalotarajiwa kuanza Mei 6 hapa hapa kwenye maskani ya nyumbani.



Naye Rais wa shirikisho hilo Leodegar Chilla Tenga alisema wachezaji wa Stars hawatashiriki michuano hiyo, kwa sababu watakuwa katika michakato ya kuvaana na mechi dhidi ya Uganda na Mauritius.

Tenga alisema Wachezaji walioko Taifa Stars hawatashiriki kwenye Taifa Cup, hivyo mikoa isije kujumuishe majina ya wachezaji hao.

Alisema hiyo ni kutokana na ukweli kwamba wakati Taifa Cup inaendelea, timu ya taifa itakuwa kambini ikijinoa kwa kupambana na mchezo wa marudiano dhidi ya Uganda na pia mchezo wa Mauritius.

Stars inatarajiwa kuingia dimbani na Uganda Mei 3 ndani ya uwanja wa CCM Kirumba, katika mechi ya raundi ya pili ya michuano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Alisema fainali hizo za Kombe la Mataifa Afrika zinatarajiwa kufanyika hapo mwakani Ivory Coast.




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.