Wakenya washtukiwa kwa mauaji TZ.
Raia wa Kenya wametiwa mbaroni mkoani Mara wakihusishwa na tuhuma za mauaji ya albino.
RC Mara Luteni Kanali Issa Machibya, alisema Wakenya hao, Eli Kiranga na Mung`are Nyandukwi, wamekamatwa na polisi kwa madai ya kumuua Winfrida Giayati Oluoch mwezi uliopita.
Alisema Wakenya hao wanatuhumiwa kumuua mwanamke huyo saa 7:00 usiku nyumbani kwake maeneo ya Sirari wilayani Tarime Machi 3 mwaka huu.
Polisi mkoani Mara imepiga marufuku waganga wa jadi kutoka Kenya, Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC ) na wale wanaotoka mikoa mingine kuigia Mara kwa kuwa wengi wao wanadaiwa kuchangia mauaji ya albino yanayoendeshwa na imani za kishirikiana za kutafuta utajiri.
Alisema tangu kuanza mwezi huu maalbino wawili wameuawa ambapo waganga wa kienyeji wanasakwa na polisi mkoani hapa wakihusishwa na mauaji ya mwanamke mmoja yaliyotokea Jumanne iliyopita katika kijiji cha Bwai Kwitururu, maarufu kama 'Paris', Musoma vijijini.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala