Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
Madenti std 3, watundikwa mimba.

Wanafunzi wanne wakiwamo wawili wa darasa la tatu katika Kata ya Mazingara Mkoa wa Tanga, wameacha shule kwa kutundikwa mimba.

Madenti hao ni wa shule za msingi Gumbonneka, Suwa, darasa la saba Shule ya Amani na wa kidato cha pili katika Sekondari Mazingara.

Afisa mtendaji wa kata hiyo ya Mazingara, Lughundi Hassan, alisema kuwa, wanafunzi hao walibainika kuwa na ujauzito huo baada ya kupimwa na wataalamu wa afya katika zahanati ya kijiji cha Mazingara.

Lughundi, alisema wanafunzi hao ni kati ya sita, waliofikishwa katika ofisi yake,baada ya kufanyiwa uchunguzi ndipo wawili kutoka Kijiji cha Amani hawakukutwa na ujauzito.

Watoto wale wa darasa la tatu walikiri kuwa na ujauzito mbele ya wazazi wao, alisema Lughundi .



 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.