Timu ya Ukaguzi yang'ara
Timu ya Netiboli ya Ukaguzi ya hapa jijini iliweza kufuata nyayo za kaka zao katika soka, baada ya kuibugiza RAS Shinyanga matonge 26-24 katika mchezo uliochezwa kwenye dimba la Kumbukumbu ya Samora hapa mjini.
Changamoto ya ushindi kwa malkia hao wa Ukaguzi ni mfungaji (GS), Eliza Musoma na mlinzi (GD), ambaye alikuwa ni Schola Nicholaus ambaye aliweza kuwa kikwazo kwa washambuliaji wa RAS Shinyanga.
Katika mchezo wa soka uliofanyika mwishoni mwa wiki Ukaguzi pia iliikandamiza RAS Shinyanga kwa mabao 2-1.
Malkia hao wa Ukaguzi wanatarajiwa kuumana na Watoto wa Nyumbani, CDA ya Dodoma.
Michuano ya Mei Mosi kitaifa inaendelea kutimua vumbi mjini hapa kwa kushirikisha michezo mbalimbali ikiwamo Netiboli, Soka, kuvuta kamba na mingineyo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala