Ushirikina waibukia kwa maticha.
Sakata la walimu kukatwa mapanga katika Wilaya za Bukombe na Kahama mkoani Shinyanga, limechukua sura mpya baada ya kukutwa wamelazwa nje ya nyumba zao usiku kwa kile kinachodaiwa ni imani za kishirikina.
Mmoja wa maticha hao anayefundisha katika Shule ya Msingi Kashero Wilayani Bukombe, Charles Bundala, alisema unapofika muda wa kulala nyakati za usiku, wanatolewa nje ya nyumba zao bila ya wao kujua.
Mwalimu huyo aliendelea kuchonga kuwa walimu zaidi ya watatu katika shule hiyo wamekwisha kufanyiwa vitendo vivyo ambavyo vinawatia hofu ya kufundisha na kundelea kuishi katika mazingira hayo.
Alisema mpaka sasa walimu zaidi ya tisa wamehamia mjini Ushirombo, umabli wa kilometa 30 kutoka katika shule za kulazimika kukatiza vipindi ili kuwahi kuondoka kurudi nyumbani kwao.
''Walimu wote wamehamia mjini na kubaki mwalimu mkuu tuu huku wengine wakitishia kuhama kabisa kufundisha shuleni hapo,'' alisema Bundala.
Hivi karibuni kumezuka vitendo vya ukataji wa mapanga kwa Walimu wanaofundisha katika shule za msingi na sekondari katika Wilaya za Bukombe na Kahama.
Vitendo hivyo, vimezua hofu kwa walimu kufundisha katika shule hizo huku wengine wakitaka kuhama katika wilaya hizo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala