Tz ya 7 kwenye Golf!
Hatimaye Timu ya Taifa ya mchezo wa Gofu ya Tanzania, sasa imeanza michuano ya mchezo wa Kombe la Challenge Afrika kwa kunyaka nafasi ya saba katika siku ya kwanza ya michuano hiyo.
Michuano hiyo iliweza kujumuisha nchi zipatazo 17 na leo inaingia siku ya pili ya michuano hiyo na kuweza kumalizika hapo kesho katika Viwanja vya Katamaya Height Golf and Tennis Resort ya mjini Katamaya.
Pia michuano hiyo ni ya viwanja 54 na Tanzania iliweza kujitwalia nafasi hiyo baada ya kukusanya jumla ya mikwaju 168, kutoka kwa mchezaji namba moja nchini Sophia Viggo aliyepiga 81 akiwemo na Hawa Wanyeche aliyejikusanyia mikwaju 87.
Kwani kila nchi imeruhusiwa kuchezesha wachezaji watatu kwa kila raundi, kwani yanahesabika matokeo ya wachezaji wawili tu waliofanya vizuri zaidi.
Mchezaji mwingine wa Tanzania ni Betty Malaba ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mchezo huo kwa upande wa wanawake nchini (TLGU), kwani kufanilkiwa kufanya vizuri katika siku ya kwanza ya michuano hiyo.
Kwani wachezaji wa Tanzania walikuwa na nafasi ya kufanya vizuri zaidi ya hapo, lakini walipata shida katika kusukuma mpira kwenye shimo ndani ya uwanja ‘putt’.
Nchi nyingine za Afrika Mashariki yaani Kenya waliweza kukamata nafasi ya sita kwa mikwaju 164 kutoka kwa Merry Karano na Josephine Ainley, ambao kila mmoja alipiga mikwaju 82 huku Uganda ikiwa katika nafasi ya tisa kwa mikwaju 171 kutoka kwa Flaviana Namakule 82 na Eva Okatch aliyepiga 89.
Kwa upande wa nchi nyingine na mikwaju waliyopata Zimbabwe (160), Namibia (160) Botswana (169), Nigeria (171), Morocco (175), Ivory Coast (175), Ghana (1820, Gabon (185), Senegal (188), Togo (214) na Angola.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala