Tafuta DHWTangazaTuandikie
   
UK yawatengea wabongo mshiko.

Balozi wa Uingereza nchini, Phillip Parham amesema nchi yake imetenga mbovu zipatazo Sh22 trilioni kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu kwenye nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania, katika kipindi miaka saba.

Akizungumza katika utoaji zawadi kwa wanafunzi bora walioshinda katika uandikaji wa insha kwa kutumia lugha ya kiingereza na kuongea kingereza fasaha, Parham alisema fedha hizo zitasaidia kuboresha elimu pamoja na ufahamu mzuri wa lugha ya kiingereza.

Alisema elimu ndiyo mwanzo wa haki, amani na furaha katika taifa lolote duniani, ndiyo maana serikali yake imeamua kutumuia fedha hizo kusisaidia nchi zinazoendelea ili kuinuia kiwango elimu kwa watu wake.

Naye Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe alisema wanafunzi wengi wahawana uwezo wa kuzungumza kiingereza fasaha, hivyo kuwafanya hata watalii wengi kushindwa kutembelea maeneo mbalimbali kwa kukosa watu wa kuwangoza.

Alisema kutokana na hali hiyo shule zitaendelea kutumia lugha ya Kiingereza kama lugha ya kufundishia wanafunzi kwa shule za sekondari na vyuoni ili kuwasaidia wanafunzi waweze kufanya vizuri katika lugha hiyo.

Katika mashindano hayo, jumla ya wanafunzi sita kutoka Tanznia Bara na Zanzibar walipatiwa zawadi mbalimbali zikiwemo Redio kubwa, kompyuta, tuzo na vyeti kutoka kituo cha Mafuta makao Mkuu ya BP.




 Gonga hapa kutoa maoni yako kuhusu story hii...!!!
 Gonga hapa kusoma maoni hayo...!!!

 Mtumie Rafiki |   Print nakala

 

Archive/Kumbukumbu:


Copyright © 2007 Darhotwire.com All rights reserved. Design by Infocomtechnologies Limited.