Walimu wasitisha mgomo kwa masharti
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kimesitisha mgomo wake uliopangwa kufanyika Mei Mosi mwaka huu badala yake utafanyika Julai 21 kama serikali itakuwa haijakamilisha kulipa deni lililobaki.
Rais wa chama hicho Bw.Gratia Mkoba, alisema CWT imefikia uamuzi huo baada ya kuona serikali ina nia ya kulipa deni hilo.
Bw. Mkoba, alisema wamesitisha mgomo huo ili kuipa nafasi CWT kukusanya madeni mapya yalioachwa katika uhakiki uliofanywa Februari mwaka jana.
Alisema zoezi la kufanya uhakiki huo litaenda kwa kasi ili kiasi kitakachohakikiwa kilipwe ndani ya mwaka huu wa fedha.
"Katika kikao chetu kilichofanyika Aprili 21 hadi 23 mwaka huu tuliazimia kusitisha mgomo huo kutokana na sababu nilizozitaja hapo awali na kama serikali haitalipa madeni hayo ndani ya siku 60 walimu wote tutaanza mgomo wetu katika tarehe hiyo,"alisema
"Shilingi bilioni 8.7 iliyolipwa na serikali mpaka sasa ni sehemu ndogo ya deni ambalo walimu wanadai kwa mujibu wa tathmini ambazotunafanya mpaka sasa, mfano katika Wilaya ya Kinondoni pekee tumegundua walimu wanadai sh. bil. 2", alisema.
Awali CWT ilitangaza mgogoro na serikali kutokana na walimu kutolipwa malimbikizo ya madai yao yaliyotokana na uhamisho, matibabu, likizo na masomo na kusababisha kutangza kwa mgomo wa walimu nchi nzima .

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala