Jamani punguzeni presha -Maximo!
Naye Kocha Mkuu wa timu ya taifa Taifa Stars Marcio Maximo, aahidi timu yake kufanya vizuri katika mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Uganda.
Maximo alisema mchezo huo unatarajia kufanyika siku za karibuni, ndani ya Uwanja wa CCM Kirumba mjini hapa.
Kwa sasa timu hiyo ya taifa iko katika kampeni za kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi ya ndani (CHAN), na imefikia hatua hiyo baada ya kuitoa Harambee Stars ya Kenya kwa jumla ya matonge 2-1.
Kocha huyo alisema amejiandaa vya kutosha kwani matumaini ya kufanya vizuri yapo, na amewaomba wakazi wa Kanda ya Ziwa kuweza kujitokeza kwa wingi kuwashangilia.
Stars iliweza kutua uwanjani hapo jana ikiwa na kikosi cha wachezaji 21 wakiwemo na viongozi 7, ilishangiliwa na wananchi wakiwemo na wale wapenzi wa mpira wa soka uwanjani hapo.
Kikosi hicho kitachuka dimbani bila Athuman Idd ambaye analazimika kukosa mchezo mmoja baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwenye mchezo wa kwanza na wa marudiano dhidi ya Harambee Stars, huku timu ya taifa ya Uganda iliwasili mjini hapa ikiwa na wachezaji 16 na viongozi 6 tayari kwa mchezo huo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala