Nashukuru kurejeshwa tena-Ivo!
Kipa namba moja wa timu ya soka ya Tanzania Taifa Stars na YangaIvo Mapunda, sasa awa huru na amesharejea katika ajira yake.
Ivo alisema kwa sasa anajisikia faraja kubwa baada ya kurejeshwa tena katika kikosi cha Stars.
Alisema ingawa alikuwa nje ya dimba kwa miezi sita lakini atajitahidi kurejea katika kiwango chake, kama ilivyokuwa hapo awali.
Kipa huyo alisema hata alipokuwa akitumikia adhabu, alikuwa akijifua mchangani.
Mbali na kufungiwa kwake binafsi alikuwa anajifua na hivyo baada ya muda atarejea katika kiwango chake, kuendana na kiwango cha wachezaji wenzake.
Mapunda na mwenzake Shadrack Nsajigwa wamerejeshwa Stars siku chache baada ya kumaliza kifungo cha miezi sita, walichokuwa wameadhibiwa na klabu yao ya Yanga kwa utovu wa nidhamu.
Kuhusu nafasi yake ya kipa namba moja Stars Ivo alisema suala la kupangwa au vinginevyo, liko mikononi mwa Kocha Mkuu wa timu hiyoMarcio Maximo.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala