Wafanyakazi wamrushia dongo RC.
RC Dar es Salaam, Bw. Abbas Kanodoro, alitolewa uvivu na
wafanyakazi kwa kutoonyesha ushirikiano na sekta za umma na binafsi Jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi hao, waliamua kutoa shutuma hizo hadharani, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Tamko la wafanyakazi hao, lilisomwa kwenye risala iliyowasilishwa na Katibu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, (TUCTA), mkoani Dar es Salaam, Bw. Everest Mwalongo.
Alisema hali ya mahusiano inatetereka kwa sababu ya kutokutana angalau mara moja kwa mwaka, kujua shughuli za kila upande, hasa kutatua matatizo ya wafanyakazi na shughuli za kijamii katika mkoa.
Bw. Mwalongo, alisema wafanyakazi hao walizoea kufanya kazi kwa karibu na Mkuu wa Mkoa kwa miaka mingi, tofauti na ilivyo hivi sasa.
Kauli hiyo, ilimfanya Bw. Kandoro `kujibu mapigo` kabla ya kusoma hotuba aliyoiandaa kwa ajili ya maadhimisho hayo.
Alikanusha kutokuwa tayari kukutana na wafanyakazi, badala yake alisema hali hiyo ipo dhidi ya viongozi wa wafanyakazi.
``Si kweli kwamba mimi sina mawasiliano na wafanyakazi,
inawasiliana nao sana, labda mngesema siwasiliani na viongozi wa wafanyakazi, hilo ningelikubali,`` alisema.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala