Chenge azushiwa
Aliyekuwa Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge
amezushiwa jambo, kuwa amejaribu kujiua kwa kunywa
sumu.
uvumi huo ulianza kuenezwa usiku wa kuamkia jana kuwa
Chenge ambaye ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM),
baada ya kunywa sumu, alikimbizwa katika Hospitali ya
Kuu ya Jeshi ya Lugalo, Dar es Salaam ambako alikuwa
taabani.
Baadhi ya ujumbe wa simu uliotumiwa watu mbalimbali
kuulizana suala la mbunge huyo, ulikuwa hivi, “Hi,
bosi ameambiwa Chenge kala sumu yupo Lugalo. Habari
zimemfikia Bosi ameshakufa,” Hebu fuatilia amekunywa
sumu na amekufa,”
Chenge alijiuzulu uwaziri baada ya kutuhumiwa kuwa
alihusika kwenye rushwa ya rada ambayo Tanzania
iliuziwa na Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza kwa
gharama ya zaidi ya Sh bilioni 65.

Gonga hapa kutoa
maoni yako kuhusu story hii...!!!

Gonga hapa kusoma
maoni hayo...!!!
Mtumie Rafiki |
Print nakala